WAZIRI MKUU KUZINDUA SAMIA LEGAL AID JUNI 16, 2025 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM, RC Chalamila wataka wananchi wenye changamoto za masuala ya kisheria kujitokeza



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid) kwa Mkoa wa Dar es Salaam Juni 16, 2025 katika viwanja vya Maturubai Mbagala Wilaya ya Temeke.

Hayo yamebainishwa leo Juni 13, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na waandishi wa habari ambapo  amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni hiyo kuanzia Juni 16 hadi Juni 25, 2025  kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za kisheria ikiwemo migogoro ya ardhi na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Kwamba Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na Wizara ya Katiba na sheria kwa udhamini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia na inafahamika kama Mama Mama Samia Legal Aid Campeign ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa katika viwanja vya Maturubai Mbagala Wilaya ya Temeke jijini humo

RC Chalamila amesema Kampeni hiyo itawasaidia wananchi kushughulikia kero na changamoto za kisheria ili kuleta haki,usawa,amani na maendeleo hivyo amewataka wananchi wenye changamoto za kisheria kujitokeza

Amesema kuwa kampeni hiyo baada ya kuzinduliwa kwenye Viwanja vya Maturubai Mbagala jijini humo itakwenda kwenye Wilaya zote za Mkoa huo.

Aidha RC Chalamila amesema ndani ya jiji hilo mbali na migogoro ya ardhi kumekuwa na matukio ya ukatili wa kijinsia hivyo kutakuwa na wataalamu wa sheria na madawati ya kijinsia ili lengo la Rais Dkt Samia kuendesha kampeni hiyo liweze kufanikiwa

Kwa upande wa Mkurugenzi wa huduma za kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema kuwa kampeni hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2023 na imefika kwenye mikoa mitano ya Zanzibar na mikoa 25 ya Tanzania bara ikiwa tayari imefikia na kusaidia zaidi ya wanancni milioni 2.

Post a Comment

0 Comments