NA MWANDISHI WETU
KADA wa Chama cha Mapinduzi Aziza Songambele amechukua fomu ya kutia nia kuwania udiwani wa Viti Maalum Kata ya Mwananyamala, Halmashauri ya Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 1, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu hiyo ameomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kumpatia na fasi ili kuwatumikia wananchi.
Kwamba ametia nia hiyo ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Mgombea huyo amechukua fomu katika ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, ambapo amekabidhiwa na Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo, Haziati Juma
0 Comments