NA MWANDISHI WETU
MFANYABIASHARA na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Godwin John Kamala amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya Chama chake kugombea Ubunge Jimbo la Kawe, Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 1, 2025 mkoani Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Kamala, amesema amechukua fomu hiyo kwa sababu CCM imetoa fursa kwa wanachama wenye nia na sifa za uongozi kutimiza wajibu wao wa kuomba kugombea.
Amesema kuwa ametia nia kugombea katika Jimbo la Kawe kwa sababu ni eneo analolifahamu na changamoto zake ameziishi na hivyo anazifahamu, anachohitaji ni fursa ya kuweza kuzishughulikia kwa maendeleo ya wana Kawe.
Kamala, amekabidhiwa fomu na Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.
0 Comments