JESSICA: MADARASA YA UONGOZI YA UVCCM YAZAA VIONGOZI CHIPUKIZI


NA MWANDISHI WETU

Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Jessica Mshama, amesema kuwa madarasa ya uongozi yanayoendeshwa na UVCCM yameendelea kuwa chachu ya kulea na kuibua viongozi wapya nchini.

Akizungumza katika mahojiano maalum na watangazaji wa kipindi cha Sentro kinachorushwa na Clouds TV, Ndg. Mshama alisema kuwa programu hizo za mafunzo zimeanza kuonyesha matunda kwa vitendo, kwani baadhi ya wahitimu wake wameanza kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.

"Madarasa haya yamekuwa daraja la kuwaandaa vijana kwa vitendo, siyo tu kwa elimu ya uongozi bali pia kwa kuwawezesha kuwa na ujasiri wa kugombea nafasi na kushiriki katika mchakato wa maamuzi," alisema Ndg. Mshama katika mahojiano hayo yaliyofanyika jana, Julai 8, 2025, katika studio za Clouds TV, jijini Dar es Salaam.

Aidha, alieleza kuwa UVCCM itaendelea kuwekeza katika kuwaandaa vijana kuwa viongozi bora, wenye maadili, uzalendo na uwezo wa kuchochea maendeleo ya taifa

Post a Comment

0 Comments