Mbeto :Katiba mpya ni ahadi ya Rais Dk Samia, ampongeza Dk Nchimbi kuwakumbusha Watanzania



Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimesema ahadi ya kupatikana  katiba mpya Tanzania iko pale pale kwakuwa ni ahadi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kabla hajaondoka madarakani  mwaka 2030.

Aidha, CCM kimeupongeza msimamo  uliotolewa na Makamu wa Rais Dkt Emmanuel Nchimbi kusisitiza azma kuandikwa katiba hiyo.

Kauli hiyo imetamkwa na katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar, Idara ya itikadi,  Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyesisitiza  katiba mpya ni ahadi ya CCM  kwa Watanzania.

Mbeto alisema Rais Dk Samia alitoa ahadi hiyo katika mkutano wa uzinduzi  kampeni za Uchaguzi  Mkuu za ccm zilizofanyika  viwanja vya Tanganyika Packers, Jijini Dar es Salaam. 

Alisema kauli ya Dk Nchimbi ni msisitizo wa dhati kufuatia maamauzi  ya ccm na  serikali zake ,hivyo  matamshi yake yanakwenda sambamba na ahadi ya Rais Dk Samia. 

"Kwa dhati kabisa nipende kumpongeza Makamu wa Rais Dk Nchimbi  kuwakumbusha Watanzania ahadi ya Katiba mpya. CCM na Kama vilivyoruhusiwa vyama vingi  katiba  itapatikana"Alisema Mbeto. 

Aidha, Katibu huyo Mwenezi, aliwataka watanzania kuendelea kuiamini CCM kwakuwa  ni chama kinachopitisha maamuzi magumu bila jazba,pupa au kwa shinikizo .

"Maamuzi yoyote yanayobeba maslahi  ya Umma   hayafanyiki kwa kiherehere.Lazima kufanyike tathmini  za kina ,uchambuzi wa kutosha huku mkizipitia faida na hasara za maamuzi husika " Alieleza.

Katibu Mwenezi  huyo,alisema inapotamkwa kauli ya  Rais, Makamu wa Rais au Waziri mkuu, kauli hiyo hutokana na utatu wa kimaamumuzi ya  chama, serikali kwa mujibu wa  vikao.

"Katiba iliopo ya Tanzania ya mwaka  1977 ni katiba bora sana.Ingekuwa si katiba bora Taifa lisingefikisha miaka zaidi ya sitini.Ni uamuzi wa watanzania wenye kupata katiba nyingine au la"Alisisitiza.

Mbeto aliendelea kufafanua kuwa jukumu la kupatikana katiba halihitaji kikiri zinazoweza kuhatarisha Amani na Utulivu, badala yake ni mambo ya kujadiliana kwa njia za kiungwana. 

Akielezea kwa undani, Mwenezi huyo alisema jukumu la kuandikwa kwa katiba mpya si la Mashirika hiari ya kijamii, watetezi wa Haki  za binadamu,upinzani au nchi washirika bali ni la watanzania wenyewe.

"Ahadi na hatma kupatikana katiba mpya iko mikononi mwa watanzania wenyewe.Dhamana ya serikali  za CCM ni kuandaa mazingira bora na wezeshi ili kupata katiba inayokidhi haja na matakwa ya nyakati "Alifafanua

Post a Comment

0 Comments