NA MWANDISHI WETU
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) John Mwita, amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama kuwania ubunge Jimbo la Kawe wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 2, 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi fomu hiyo, Mwita amesema ametimiza wajibu wake wa kidemokrasia na haki yake ya kikatiba kama raia mwenye wajibu wa kushiriki katika uongozi wa Taifa kwa kugombea nafasi ya uongozi.
Hata hivyo ameeleza kuwa baada ya kurejesha fomu hiyo kinachobaki ni kusubiri taratibu nyingine za Chama ili kuamua nani atakayepatiwa nafasi ya kuliwakilisha Jimbo la Kawe.
Mwita, amekabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Amos Richard.

0 Comments