MWANAFUNZI VETA ACHORA RAMANI ZA NYUMBA KWA MGUU, ni mlemavu wa mikono, aishauri jamii kutowaficha watoto......






NA MWANDISHI WETU

MWANAFUNZI wa Mwaka wa pili wa Chuo Cha Elimu na Ufundi Stadi (VETA) Dodoma Joseph Mtei ambaye ambaye ni mlemavu wa mikono akisomea fani ya uchoraji wa ramani za nyumba amesema kwa sasa anauwezo wa kuchora ramani ya aina yoyote kwa kutumia mguu.

Mtei amebainisha hayo Julai 4, 2025 akizungumza na waandishi wa habari katika banda la VETA kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es salaam.

Hivyoa ametumia fursa hiyo kuishauri jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu nabadala yake wawapeleke VETA wapate ujuzi utakao wasaidia kujikwamua kiuchumi.

Ameishukuru VETA kwa kumkubalia  kujiunga na chuo hicho kwa ajili ya kupata ujuzi huu, kwani walimpa fursa ya kupata ujuzi huo licha ya kuwa ni mlemavu.

"Nashukuru VETA kwa kunipokea, kwani hawakuona kwamba mimi ni mlemava ambaye sina mikono labda nitakua mzigo kwa walimu walinichukulia kama wanafunzi wewengine," amesema Mtei.

Ameeleza kuwa alianza masompo VETA Mwaka wa kwanza 2024 na sasa yupo Mwaka wa pili,  hivyo anayo furaha kwa sasa kwamba anao uwezo wa kuchora ramani ya nyumba aina yoyote, hivyo kumfanya kutokuwa tegemezi.

Aidha amesema amekuja katika maonesho ya Kimataifa ya kibiashara maarufu kama Sabasaba kuwaonesha Watanzania wenzake kuwa wasiwafiche watoto wenye ulemavu,au wale wana viungo vyote lakini wamekata tamaa kwa kuona kwamba hawawezi kufanya chochote wanaweza kujiunga na VETA nakupata ujuzi wa fani mbalimbali. 

"Wakija VETA hawawezi kukosa cha kufanya,watafanya kila kitu kwasabubu kama darasani wameona hakuna Cha kufanya,VETA wanafundisha kwa vitendo kwani hawa angalii uelewa wako wa darasani wana angalia matendo yako ambayo yatakufanya uweze kufanya kile ambacho wewe una uwezo nacho."amesema Joseph

Nakuongeza kuwa "Kwa mfano mimi hapa nimeenda VETA nikiwa sijui kabisa kuchora ramani za Majengo ila kwa vile walinipa Mafunzo na ujuzi sasa hivi nina uwezo wa kuchora ramani ambayo naweza nikaiuza kabisa nikapata kipato".

Hata hivyo Mtei amesema kwamba ramani haiwezi kuchorwa kwa siku moja na kuimaliza, inachukua muda, ili ramani ikamilike unaweza kutumia wiki moja,mbili hadi wiki tatu.

Post a Comment

0 Comments