Na Victor Masangu, Kibaha
Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amerejesha leo fomu rasmi kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge Jimbo hilo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na madiwani wote ambao wameteuliwa katika kuleta mabadilko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali.
Akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi pamoja na viongozi mbali mbali ambao wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumsindikiza katika zoezi hilo la urudishaji wa fomu amebainisha kwamba endapo atapata fursa ya kuchaguliwa tena katika nafasi hiyo ataendeleza kusikiliza kero na chanagmoto za wananchi na kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha Koka amesema kwamba kwa sasa wanachama wote wa CCM wanapaswa kumpa ushirikiano wa kutosha kwa lengo la kuweza vunja makundi na kushikamana kwa pamoja lengo ikiwa ni kuweza kumpa kura nyingi za kishindo kwa nafasi ya Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge pamoja na nafasi ya udiwani.
"Nawashukuru sana wana ccm wote wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kuweza kuniamini na kunipa kura nyingi katika mchakato wa kura za maoni na leo hii nimeweza kupata fursa y kuweza kurejesha fomu kwa ajili ya kuweza kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kbaha mjini naa kwamba taratibu zote zimekwenda vizuri na fomu zote ambazo zinastahili tayari nimeshazirejesha,"amebaisha Koka.
Aidha amebainisha kwamba kwa sasa hivi kitu kikubwa ni kuhakikisha wanawekaa misingi imara ambayo itaweza kuleta maabadiliko makubwa katika suala zima la kuweza kupata kura nyingi za kishindo katika kuelekea uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu wa 2025.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Nyamka amesema kwa sasa zoezi la mchakato wa kura za maoni tayari umeshamlizika hivyo wagombea walioshindwa pamoja na wanachama wote kuvunja makundi yote na kuwa kitu kimoja lengo kubwa ni kuwa na nguvu ya pamoja ambayo itasaidia kuweza kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu.
0 Comments