Mbeto asema walichokipanda ACT Wazalendo ndicho watakachovuna


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimekitaka ACT  Wazalendo kisimtafute mchawi katika sakata la kuenguliwa mgombea wao wa urais , badala yake wajue  kinachopandwa ndicho kinachovunwa.

Pia kimemtaka Kiongozi Mstaafu wa chama hicho  Zito Kabwe kuacha kutoa shutuma zisozo na  sababu wakati  Luhaga Mpina ameengulia kwa kukiuka  masharti ya  katiba  ya chama hicho.

Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar  Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis  Mbeto  Khamis ameeleza hayo na kusema yaliowakuta ni matokeo ya dhulma aliofanyiwa  Kiogozi wa chama hicho Doroth Semu kwa  kulazimishwa ajitoe kuwania Urais  .

Mbeto  alisema tayari ACT  walishateua jina la  mgombea wa urais  lakini kutokana na mizengwe ya viongozi  watatu wa chama ndiko kulikoleta  kizaazaa chote

Aliwataja viongozi hao ni Makamu Mwenyekiti  ACT Wazalendo  Ismail Jussa Ladhu  ,Mwanasheria wao Ramadhan Said Shaaban na Zito Kabwe ndio waliosabisha yotekee yalitokea

"Vigogo  watatu wa ACT Wazalendo wamehusika kuvunja katiba  ya chama hicho. Walidhani wanachama  ni mbumbumbu wa Katiba. Kuvunja katiba kwa maslahi binafsi ni  zaidi ya udikteta  " Alisema Mbeto 

Aidha, Mbeto alimtaka Zitto awe  mkweli kwa  kukosea na  kuacha kuitupia  lawama CCM wakati  anajua fika waliokitosa chama hicho  kikose mgombea urais ni yeye na wenzake  .

"ACT kiache upotoshaji . Zito anapodai CCM imemzuia Luhaga Mpina ni madai ya kitoto na  kipuuzi .Aliyekuwa Mwenyekiti  wa CCM  mkoanj  wa Arusha Dk Godfrey  Malisa ameshitaki Mahakama Kuu .Je  ametumwa  na Zito  au Jussa "Alihoji Mwenezi  huyo .

Mbeto  amekitaka ACT  hicho kwanza kuheshimu  matakwa ya katiba yake ,kifuate taratibu na  kikanuni bila kuamua mambo kwa mihemko au kwa  upendeleo .

"Hii ni mara ya Pili  viongozi wa ACT  wanafanya maamuzi kwa pupa na batili .Mwaka 2020 kilimdandia Marehemu Bernad Membe na kumtaka  awanie  urais kisha  vigogo  wa ACT wakagoma kumfanyia kampeni" Alikumbusha

Hata hivyo Mbeto  alihoji  sababu za kuliondoa jina la Dorothy ambaye  alipitishwa na mkutano  Mkuu wa  Taifa  wa ACT kama ambavyo  mgombea urais wa CCM Rais  Dk  Samia Suluhu  Hassan alivyoidhinishwa

"Jussa na Zito  ni madikteta  uchwara  wasiothamini Usawa wa Kijinsia . Wametumia ubabe kuliondoa jina la  mgombea halali ili kumpandikiza mgombea  asiyekidhi matakwa ya katiba pia akiwa hana  sifa ya uanachama  wake " Alisisitiza Mbeto.

Post a Comment

0 Comments