MBETO ATABIRI ANGUKO LA OTHMAN UCHAGUZI WA URAIS ZBAR


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar  

Chama Cha Mapinduzi   kumemtaja  Mgombea Urais wa ACT  Wazalendo , Othman Masoud Othman, atashindwa vibaya katika kinyang'anyiro cha Urais  kutokana na  uwezo wake kuwa mdogo mbele ya mgombea  CCM  Rais Dk Hussein  Ali Mwinyi .


Pia CCM kimemtaka Othman kujua  kuwa Upigaji  Kura kwa siku  mbili si suala la  kisiasa, hadithi na  simulizi bali lipo kwa mujibu  wa sheria . 

Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar  , Idara ya Itikadi, Uenezi  na Mafunzo , Khamisi  Mbeto  Khamis ameeleza hayo huku akimtaka ajiandae kisaikolojia  kushindwa vibaya katika Uchaguzi  wa oktoba  Mwaka huu.

Mbeto  alisema kama yupo  mgombea toka upinzani  atakayepata matokeo ya kura chache na kuingia katika kurasa za  historia  ya Chaguzi kuu za Vyama vingi Zanzibar  toka Mwaka 1957 hadi 2025 ni Othman.

Alisema atapata matokeo ya aibu kwakuwa si kiongozi  wa kisiasa  mwenye historia pia rekeodi ya  kutumikia wananchii, badala yake amejiingiza  katika  siasa kwa kushinikizwa na utashi wa  wapambe .

"Othman  atashindwa vibaya  Urais kwasababu hayumo katika vitabu vya  historia  ya  siasa za Zanzibar .Ni mgombea   dhaifu kuwahi kutokea . Kama si ushabiki , mizengwe na udalali wa wapambe alikataa kugombea Urais " Alisema Mbeto

Katibu  huyo  Mwenezi  alisema  Othman akitaka kujua  kama ataanguka vibaya katika Uchaguzi  wa mwaka huu,atazame idadi ndogo ya wanachama wa ACT  waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu  ya urais .

'Dalili ya mvua huanza kutanda  mawingu .Nyota njema huonekana  mapema asubuhi. Kwa hali ya manung'uniko na wanachama kususia  ndani  ya ACT  Othman ataanguka vibaya ifikapo Oktoba "Alieleza 

Mbeto  alisifu juhudi za utendaji  uwezo binafsi   ,umakini na utayari wa mgombea wa CCM  Dk Mwinyi pamoja na utumishi  wake wa miaka mitano  iliopita alivyoiletea Zanzibar maendeleo  ya haraka. 

"Tumejiandaa kisawasawa na sasa tupo tayari kwa kupiga kura .Hatuingii katika uchaguzi  huu kwa kubahatisha  .Mgombea wetu lazima ashinde" Alisema Katibu  huyo Mwenezi.

Post a Comment

0 Comments