Mbeto: Hakuna cha kuzuia ushindi wa CCM Zanzibar 2025-2030


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimesema kitashinda Uchaguzi Mkuu  wa Oktoba Mwaka  huu kwa mujibu  wa sheria na taratibu za kidemokrasia kwani   hakuna  sababu ya   CCM  kushindwa  Visiwani  Zanzibar .

Katibu wa Kamati  Maalum  ya  Nec Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo  ,Khamisi  Mbeto  Khamis, ameeleza hayo baada ya mgombea  Urais wa CCM, Rais  Dk Hussein  Ali Mwinyi alipohutubia maelefu ya wana CCM na Wananchi.

Mkutano  wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM   kwa Zanzibar ,zimezinduliwa katika Uwanja wa Kumbukumbu  ya Mwenyekiti  Mao Tse Tung,  Kisiwani Unguja. 

Mbeto  alisema  Ushindi wa CCM  hauna  kizuizi  chochote  baada ya serikali ya Awamu  ya Nane kutimiza wajibu wa kuwatumikia  wananchi chini  ya serikali ya  Rais Dk Mwinyi. 

Alisema haiba  ya Ustawi wa Maendeleo  inayoonekana Unguja na Pemba  ,ni  tiketi  itakayokipatia Ushindi wa  kishindo  CCM Mwaka 2025-2030.

"CCM hakina sababu  ya kushindwa Uchaguzi    huu . Kimetekeleza kwa vitendo Sera zake   kwa ufanisi na viwango stahili " Alisema Mbeto 

Aidha, Katibu  huyo Mwenezi  ,aliongeza kusema kwa CCM  ni  fahari kuona idadi kubwa ya Wananchi,  wakiendelea kukiunga mkono  , kukuamini  , kukipenda na kukitegemea .

"Siri ya ushindi  wa chama chochote makini  cha Siasa   ni maandazi ya kimkakati  , kioganaizesheni na  kujipanga .Tumejiandaa kisawasawa  ,sasa   tuko tayari kwa ushindi wa kidemokrasia " Alieleza 

Katibu huyo Mwenezi  akijigamba mbele ya  Waandishi  wa habari, amesifu kazi kubwa iliofanywa na SMZ, miaka mitano iliopita  chini ya  Utawala wa Dk Mwinyi.

Alisema CCM kitashinda kwa Asilimia  85  ya kura za Urais,  hivyo Mgombea wake   Dk Mwinyi ,  atarudishwa tena  madarakani kwa ridhaa ya Wananchi .

"Kielelezo cha ushindi wetu  ni matokeo ya kufanikisha kazi za  kimaendeleo . Mafanikio yaliopatikana katika  Sekta  za  Elimu , Miundombinu, Ustawi wa Jamii , Miradi ya   Kiuchumi, Barabara za lami , Usafiri  wa Anga , Biashara na Utalii kwa ccm ni funguo ya ushindi  "Alisisitiza .

Mbeto alisema kimsingi Utendaji wa Serikali  ya Awamu ya Nane, umezikonga nyoyo za  Wananchi  pia kuwavutia  hata  wageni wanaotembelea Visiwani humu.

Post a Comment

0 Comments