Na Victor Masangu,Kibaha
Katibu wa siasa na uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani David Mramba amewahimiza viongozi na wanachama wote kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi tukio kubwa la kihistoria la uzinduzi rasmi wa kampeni ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 28 katika viwanja vya Tanganyika Peckars jijini Dar es Salaam.
Mramba ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho kuhusiana na uzinduzi huo ambapo amesema kwamba wanachama wanapaswa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuweza kumsapoti Rais Dkt. Samia kwani ameweza kufanya mambo makubwa katika suala zima la kutenga fedha kwa ajil ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
" Kwa kweli sisi kama chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani tumejipanga kushiriki kikamilifu katika tukio kubwa la uzinduzi wa kampeni kitaifa ambazo zitafanyika Jijini Dar es Salaam na kwamba kitu kikubwa ninachowaomba viongozi na wanachama wote kujitokeza kwa wingi ikiwa ni pamoja na kusikiliza utekelezaji wa Ilani,"amebainisha Mramba.
Aidha Mramba amebainisha kwamba hatowavumilia baadhi ya wanachama ambao wamekuwa na tabia ya kukisaliti chama na kwamba akijatumamwanachama yoyote yule kwenda kuhamia katika chama kingine cha upinzani.
"Kumekuwepo na baadhi ya wanachama ambao ni kivuli na kuamua kukisaliti chama kwa hivyo mimi nawaomba ni lazima kuhakikisha kwamba wanazingatia kanuni na taratibu za chama.
Aidha Mwenezi Mramba wamewahimiza madiwani na wabunge wote katikaMkoa wa Pwani ambao wamepata fursa ya kuteuliwa ya kuwania nafasi zao kuhakikisha kwamba wanaweka misingi ya kupeperusha vyema bendera ya chama cha mapinduzi na kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu.
0 Comments