RAIS DKT. SAMIA KUONGOZA UZINDUZI WA HARAMBEE YA BIL. 100 ZA KAMPENI



#KAZIINAONGEA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kampeni za chama hicho, utakaofanyika Agosti 12, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wahariri na waandishi wa habari Jumatatu, Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema harambee hiyo inalenga kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 100.

Fedha hizo, amesema, zitatumika kufanikisha maandalizi ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025. Maandalizi hayo yanajumuisha ununuzi wa magari, mafuta, mabango, fulana, kanga na vifaa vingine vya kampeni.

Lengo ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na maandalizi madhubuti, ya kisasa na yanayoendana na mahitaji ya kisiasa ya sasa.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utatoa fursa kwa Watanzania kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani kwa kipindi kijacho cha uongozi.

#KazinaUtuTunasongaMbele

Post a Comment

0 Comments