THAMANI MITAJI SOKO LA BIMA YAIMARIKA, yaongezeka kutoka bilioni 906 hadi bilioni 993 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025


Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware, akizungumza katika kikao kazi kati cha Wahariri na Waandishi wa Habari na Mamlaka hiyo kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akifafanua baadhi ya Mambo katika kikao kazi hicho. 







NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan thamani ya mitaji katuka soko la bima imeimarika ktoka shilingi bilioni 416.0 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi bilioni 847.3 mwaka 2024.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 18, 2025 na Kamishna wa TIRA, Dkt. Baghayo Saqware, akizungumza katika kikao kazi kati ya Wahariri na Waandishi wa Habari na Mamlaka hiyo kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, kilichofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amesema hilo ni sawa na jumla ya ongezeko la asilimia 103.7, ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 26.3 kwa mwaka.

Dkt. Saqware amesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, thamani ya mitaji katika soko la bima iliongezeka kutoka shilingi bilioni 906 mwaka 2024 hadi bilioni 993 kufikia Juni 30, 2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.5.

Ameongeza kuwa katika kipinchi hicho cha mika minne ya uongozi wa Dkt. Samia idadi ya watoa huduma za bima imeongezeka kutoka 993 mwaka 2021 hadi kufikia 2,425 Juni 2025 na kwamba hilo ni sawa na ongezeko la jumla ya asilimia 144.2 na kwamba ongezeko hilo ni sawa na wastani wa asilimia 22.1 kwa mwaka.

"Katika kipindi hiki pia, Mamlaka imeongeza aina mpya ya watoa huduma ikiwa ni pamoja na watoa huduma za afya (HSPs), warekebishaji na watengenezaji magari (ARMs) na Watoa Huduma Kidigitali. Vile vile, kampuni za bima mtawanyo nchini zimeongezeka kutoka kampuni moja mwaka 2021 hadi kampuni nne mwaka 2024," amesema Dkt. Saqware.

Kadhalika Dkt. Saqware amesema kuwa Serikali imeanzisha konsortiamu ya Bima ya Kilimo ili kuhakikisha uendelevu wa miradi pamoja na miundombinu, hatua inayolenga kuhudumia wakulima na kupunguza athari za majanga ya asili.

‎Kwamba konsortiamu hiyo ni umoja wa makampuni ya bima yanayotoa bima za kilimo, ambapo jumla ya makampuni 15 yameunda mtaji mkubwa kwa ajili ya kulipa fidia kutokana na majanga yatokanayo na kazi za kilimo na kwamba hatua hiyo inalenga kuongeza tija katika sekta ya kilimo na imekuwa juhudi muhimu sana kwa taifa.

‎Ameeleza kuwa Tayari wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wameanza kulipwa fidia kutokana na majanga yaliyosababishwa na mvua kubwa, huku wakulima wa pamba wakinufaika kwa kulipwa baada ya kuathiriwa na wadudu waharibifu. Hii ni miongoni mwa hatua muhimu zilizochukuliwa na Serikali ili kuhudumia wananchi.

‎Amebainisha kuwa Serikali imeanzisha konsortiamu ya Mafuta na Gesi, umoja unaojumuisha zaidi ya makampuni ishirini na mbili yaliyotengeneza mtaji wa pamoja kwa lengo la kuhakikisha sekta ya mafuta na gesi inavuna fursa zilizopo nchini.

‎Aidha amebainisha kuwa Makampuni hayo ya mafuta na Gesi yamewekeza mtaji ili kushiriki biashara ya mafuta na gesi, ambayo awali imezoeleka kufanywa na kampuni za kigeni. Kupitia umoja huu wa makampuni, Shell na washirika wake wanatarajiwa kushiriki kikamilifu katika uchumi wa mafuta na gesi wa Tanzania. Serikali imetajwa kustahili pongezi kwa kuridhia kuanzishwa kwa hatua hiyo.

‎Mbali na hayo, ameeleza kuwa hatua nyingine muhimu iliyochukuliwa na Serikali ni kuimarishwa kwa mifumo ya TEHAMA, kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia ambapo jumla ya taasisi 30 zinatarajiwa kuunganishwa ili kusomana katika mfumo huo.

Post a Comment

0 Comments