TIMU YA NETIBOLI NISHATI YATINGA KUMI NA SITA BORA MASHINDANO YA SHIMIWI




*Yawa kinara katika kundi C

NA MWANDISHI WETU

Wakati mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali  (SHIMIWI) yakishika kasi jijini Mwanza  kwa hatua za awali, Wizara ya Nishati imetinga  katika hatua ya 16 bora  katika mchezo wa Netiboli kwa kuwa na jumla  ya alama tisa (9). 

Wizara ya Nishati ipo  katika kundi C ambapo kundi hilo linaundwa na Timu ya RAS Singida, RAS Shinyanga, Wizara ya Kilimo, pamoja na  Hazina.

Awali,  Wizara ya Nishati ilitupa karata yake ya kwanza dhidi ya  RAS Singida na kuibuka na ushindi wa magoli 40 kwa 0 (sifuri), Mchezo wa Pili Nishati ilicheza na Wizara ya Kilimo na kushinda kwa magoli  34 kwa 22, mchezo wa tatu Nishati ilipoteza  dhidi ya timu ya Hazina kwa magoli 36 kwa 21, huku katika mchezo wa nne Nishati ikicheza na Timu ya RAS Shinyanga na kuibuka na ushindi wa magoli 27 kwa 19 na hivyo  kuwa kinara katika kundi C ikiwa na jumla ya magoli 122.

Aidha, Timu ya Wizara kwa sasa inasubiri  taratibu za upangaji  wa makundi ambayo yanatarajiwa kupangwa mwisho wa juma hili ambayo ni tarehe 6-7 Septemba, 2025.

Michezo  ya SHIMIWI ilianza Septemba Mosi 2025  ambapo ufunguzi utafanyika Septemba 07, 2025 na mashindano yatamalizika Septemba  16, 2025.

Katika michezo hiyo, Wizara ya Nishati imepeleka timu mbalimbali ikiwemo  timu ya mpira wa miguu, riadha, karata, draft, mchezo wa Vishale, mchezo wa bao na baiskeli.

Mashindano ya SHIMIWI yamebeba na kauli mbiu isemayo  "Michezo kwa Watumishi Huongeza Tija Kazini, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025,kwa Amani na Utulivu".

Post a Comment

0 Comments