NA MWANDISHI WETU
WANANCHI wa kata ya Kakesio iliyoko Tarafa ya Ngorongoro Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha watanufaika na mradi wa Maji kwa ajili ya Mifugo na matumizi ya binadamu kufuatia Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuchimba Kisima cha Maji chenye urefu wa mita 110 ambacho kinatarajiwa kuzalisha maji lita 80,000 kwa siku.
Uchimbaji wa Kisima hicho ni
muendelezo wa kazi nzuri inayofanya na Serikali kwa Wananchi wanaoishi katika
eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo Kisima kama hicho kimechimbwa eneo
la Mlima matiti kwa ajili ya wananchi wa Kata ya Endulen na Alaetoli na baadae
mradi kama huo utatekelezwa katika Kata ya Olbalbal ili kusaidia wananchi
kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji kwa mifugo katika msimu wote wa
mwaka.


0 Comments