Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.
Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaotembelea
eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wameendelea kufanya shughuli za utalii kwa amani,
usalama na utulivu na kufurahia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko hifadhi
ya Ngorongoro
Akizungumzia katika geti kuu la kuingia
hifadhi ya Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Idara ya huduma za Utalii na Masoko
Ngorongoro Bw. Peter Makutian amesema kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi
mkuu wa Tanzaia hadi kufikia tarehe 5 novemba, 2025 wageni takribani 1200
kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kutembelea hifadhi hiyo na kufanya
utalii.
“Ngorongoro tunaendelea kupokea
wageni katika kipindi hiki cha msimu wa wastani na tuna Imani kuelekea
kipindi cha sikukuuu za mwisho wa mwaka watalii watakuwa wengi zaidi .” alisema
Makutian.
Mmoja wa wageni kutoka Nchini Colombia
Isabella Jerónimol ameeleza kuwa ametembeleaa Tanzania akiwa na familia
ya watu 26 ambapo chaguo lao ni kuona hifadhi ya Ngorongoro kutokana na
hali ya utulivu, amani, ukarimu pamoja na utajiri wa vivutio vya utalii
vilivyopo.
Bw. Dunstan Sospeter kutoka Dar es Salaam
akiwa katika hifadhi ya Ngorongoro na Familia yake ameelezea kufurahishwa na
hali ya usalama na kushuhudia utalii wa wanyamapori, uhifadhi endelevu, Wanyama
mbalimbali ambao wanaweza kuonekana kwa pamoja katika muda ambapo pia ametumia
fursa hiyo na familia yake kutembelea Bonde la Olduvai, mchanga
unaohama na kreta ya Ngorongoro.

.jpg)

0 Comments