Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Ndugu Ado Shaibu Ado amekutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Idara na Vitendo (CMT) wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kujitambulisha na kuomba ushirikiano kwao.
Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru leo tarehe 1 Desemba 2025.
Ndugu Ado amewahakikishia wakuu wa hao wa Idara na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa ujumla kuwa atatoa ushirikiano wa hali ya juu kwao katika kuzikabili na kuzitatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa dhamana yake kama mwakilishi wa wananchi.
Kupitia kikao hicho Ndugu Ado amepokea changamoto mbalimbali kutoka kwa washiriki wa kikao hicho na kuahidi kuzifanyia kazi kwa kuwashirikisha wadau wadau wengine wa maendeleo.
0 Comments