NA MWANDISHI WETU ,KIBAHA
Diwani mteule wa Kata ya Tumbi Dkt. Nicas Mawazo amechaguliwa kuwa Meya mteule wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha baada ya kupata kura 15 kati ya kura halali zipatazo 19 ambazo zimepigwa na madiwani wateule wa chama cha mapinduzi (CCM) huku Aziza Mruma akichaguliwa kuwa katika nafasi ya Naibu meya kwa kupata kura 10 .
Akitangaza matokeo hayo ya uchaguzi wa ndani wa chama Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Mawazo amebainisha kwamba zoezi zima uchaguzi huo umemalizika salama na kwamba viongozi hao wateule wanatarajiwa kuapisha Disemba 4 mwaka huu
Katibu huyo amefafanua kuwa zoezi hilo la uchaguzi limekwenda vizuri na kwamba wagombea wote wameridhishwa na matokeo hayo na kuwahimiza viongozi hao kuvunja makundi na badala yake wawatumikie wananchi.
Kwa upande wake Meya mteule kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM ) Dr,Nicas Mawazo amesema kwamba uchaguzi huo umeendeshwa kwa haki na uhuru na kwamba matarajio yake makubwa ni kushirikiana na madiwani wenzake katika kuwaletea chachu ya maendeleo ikiwa pamoja na kuwapambania wananchi walio wanyonge.
Naye Naibu Meya mteule waa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Aziza Mruma amesema kuwa lengo lake kubwa ni kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Viongozi hao waliochaguliwa katika nafasi za Meya na Naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha wanatarajiwa kuapishwa rasmi Disemba 4 mwaka huu.

0 Comments