NA MWANDISHI WETU
Ndugu Ado Shaibu Ado, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini amesema anazirejea na kuweka bayana ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni ili wananchi waweze kumsimamia na kumwajibisha katika utekelezaji wake.
Ado alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa Kata ya Nandembo uliofanyika tarehe 2 Desemba 2024 katika Kijiji cha Nandembo.
“Wenzetu wazungu wana dhana wanaiita social contract, mkataba baina ya viongozi na umma. Kiongozi anapopewa madaraka anakuwa kwenye mkataba na umma kufanyia kazi maslahi ya umma. Mimi nawaahidi kufanya kila jitihada ndani na nje ya Bunge kufanyia kazi ahadi nilizowapa na iwapo sitafanya hivyo nawaruhusu mniwajibishe. Mimi ni mtumishi wenu, sio bosi wenu” alisisitiza Ndugu Ado
0 Comments