NA MWANDISHI WETU
Mkuu
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bi. Grace
Mghase, leo Januari 20, 2026, amemkabidhi Pikipiki aina ya Boxer Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Mundarara na Matale, Bw. Zephania Nyalyoto.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Bi. Mghase alisema kuwa pikipiki hiyo itarahisisha
utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya Jamii, hususan ufuatiliaji wa marejesho
ya mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri na usajili wa vikundi vya huduma ndogo
za fedha.
“Leo
namkabidhi pikipiki Bw. Zephania Nyalyoto, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya
Mundarara na Matale, ili imrahisishie katika shughuli za Maendeleo ya Jamii,
hususan kufuatilia urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 na usajili wa vikundi
vya huduma ndogo za fedha,” amesema Bi. Mghase.



0 Comments