MIAMBA YATEMBELEA MWAMBA WA NGORONGORO.




NA MWANDISHI WETU

Ikiwa ni majira ya Masika na kiubaridi, Bustani ya Eden ya Ngorongoro ikizungukwa na kingo zenye urefu wa Mita 610  huku wanyama na ndege wakichagiza kwa sauti murua zinazoashiria kuwa Ngorongoro ni mwamba wa miamba usiotikisika  na kusheheni msingi imara wa vivutio vya asili, urithi wa utamanuni na maajabu saba katika eneo moja.

Miamba inayounda Bodi ya Wakurugenzi ikiongozwa na makamu mwenyekiti  Dkt Harrieth Mtae inatembelea hifadhi ya Ngorongoro kuanzia ofisi za makao makuu hadi Kreta ya Ngorongoro na kujionea Eden hiyo ikiwa imesheheni kila aina ya ufahari unaoweza kuelezeka  kidunia.

Bodi hii ni sawa na miamba ndani ya Mwamba kwani imejaa wabobezi katika masuala  mengi ikiwemo ulinzi,uhifadhi, uchumi, ikolojia, maendeleo ya jamii, ukaguzi, sheria, utawala na diplomasia

Kubwa wanalilosisitiza kwa menejimenti  “mnafanya kazi nzuri endeleeni kuchapa kazi na tangazeni kitaifa na kimataifa fahari ya Ngorongoro ambayo ni kivutio bora  cha Utalii Afrika mwaka 2025

Post a Comment

0 Comments