MBETO: HAKUNA TAMKO LA CCM AU ACT NI UAMUZI WA KITAIFA


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema hakuna tamko la CCM na ACT  bali ni tamko la  mapatano ya kudumisha Serikali  ya Umoja wa Kiitaifa  Zanzibar kwa niaba ya Wananchi .

Pia kimesisitiza  tamko hilo kimsingi limezingatia  kukuza Ustawi wa Kisiasa, ,Afya na maslahi ya  pamoja katika kubeba dhima ya Maendeleo ya Wananchi .

Maelezo hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis , aliyesema tamko hilo ni matokeo  kukamilika kwa mchakato wa mazungumzo baina ya  CCM na ACT.

Mbeto akielezea kwa undani, alisema yaliomo ndani ya  tamko  hilo ,   yatasomwa kwa pamoja na  pande  zote  za kisiasa huku wananchi na dunia ikishuhudia.

Alisema ni bada ya  juhudi  za   mazumgumzo  yalioongozwa na Marais Wastaafu  Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi  Wakuu  wa CCM na ACT , kwa dhamira ya   kujenga na kuendeleza Umoja.

"Yote yaliomo katika tamko hilo  yatasomwa kwa pamoja . Msingi wa tamko hilo  ni kuendeleza Amani,  Umoja wa Kitaifa, Mshikamano, Usawa ,Haki na Maelewano"  Alisema  Mbeto. 

Aidha, Katibu huyo Mwenezi  , aliwaeleza Waandishi wa habari waliofika Ofisini kwake, huku  akilitaja tamko hilo,  limezingatia kuweka namna bora ya kuipeleka  mbele  Zanzibar  .

"Tumedhamiria kwa dhati kufanya kazi pamoja ,  kushirikiana na  kusimamia maelewano. Mahali walipo  watu wazima  haliharibiki neno  .Tuna matumaini kuliko wakati wowote " Alisisitiza Mbeto.

Hata hivyo Mwenezi huyo wa CCM aliwataka  wananchi wote wa Unguja na Pemba  kulipokea tamko hilo ,kulitegemea na kusimamia kwa madhumuni ya kuendeleza Umoja na Amani.

Post a Comment

0 Comments