MBETO: MIIKO NA USIRI WA AJENDA ZA VIKAO UHESHIMIWE ZBAR

Na Mwandishi  Wetu , Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa na kauli iliotolewa na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othmam, kwa kutaja baadhi ya ajenda  za vikao ,hatua ambayo inaweza kuathiri mustakbali wa nia njema ya  pamoja.

CCM pia kimezitaka pande zote kuelewa kuwa,kila mmoja ana wajibu wa  kulinda na kutunza siri za vikao,kanuni, maadili na miiko bila kuzungumzia ajenda ambazo hazija jadiliwa .

Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis,  aliyesema si vyema kwa   CCM  au kwa ACT kuanza kutaja ajenda za vikao vya siri  hadharani.

Mbeto alisema  hadi sasa kilichosainiwa ni kabrasha la tamko la pamoja kuelekea kuanza mjadala wa  ajenda zote zinazotakiwa kujadiliwa kwa usiri baada ya kamati ya pamoja kuundwa na kuanza kazi kwa mujibu wa hadidu za rejea.

Alisema  ni muhimu sana kwa pande zote zikaficha siri za Vikao bila kutamka hadharani kabla ya kufikiwa kwa maazimio ya  Kamati ya pamoja .

"Ni lazima Viongozi  wa pande  zote mbili wawe na kaba ya  usiri unaozingatia miiko na maadili yaliokubaliwa.Upande wowote unapokiuka  rejea za makubaliano kunaweza kudhoofisha njia safi na dhamira njema "Alisema Mbeto .

Aidha, Katibu huyo Mwenezi, alisema ni muhimu kila upande ukatambua kutakuwa na wajumbe wa  Kamati ya pamoja ambayo ndio itakayokabidhiwa  ajenda za  majadiliano.

Mbeto amemtaja Mwemyekiti wa ACT Wazalendo, Othman, kwa kutaja baadhi ya ajenda ambazo bado ni siri  na zitakazojadiliwa na Kamati ya pamoja  baada ya makubaliano ya  pamoja ya  pande  zote mbili kufikiwa.

Mbeto aliedai katika mkutano na Wanachama wa ACT Wazalendo  uliofanyika katika , Ukumbi wa mpiga dili wilaya  ya magharib B mkoa wa mjini kijiji cha kombeni, mwenyekiti wa  chama hicho alikosea kutaja  ajenda za vikao kana kwamba maamuzi hayo ndiyo yaliofikiwa.

"Tamko la pamoja si  uamuzi wala matakwa ya  upande mmoja. Jambo hili ifahamike ni nyeti lililobeba matumaini ya Wananchi.Si  tangazo linaloweza kutaangazwa na  chama kimoja kiushabiki" Alisisitiza Mwenezi  huyo.

Mbeto alisema ikiwa Viongozi wa pande mbili za kisiasa zitaacha ushabiki au kuligeuza tamko la pamoja ni mradi wa kisiasa, haitahesabika huo kama ni  uamuzi wenye mantiki na  mashiko.

"Kimsingi ndio kwanza sanduku la juhudi na Urithi wa mazungumzo ya takriban miezi minane iliopita hata  ukurasa wa kwanza  haujafunguliwa . Uzuri wa usomaji wa kitabu kichochote  msomaji  anatakiwa awe na umakini na mtulivu"Alieleza Mwenezi  huyo.


Post a Comment

0 Comments