MWENYEKITI WAZAZI TAIFA ATUA BAGAMOYO AWAASA VIONGOZI CCM KUSIMAMIA MIKOPO



Na Victor  Masangu,Bagamoyo 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  ya Wazazi Taifa Ndg. Fadhili Maganya amewasa viongozi wa CCM  kuhakikisha kwamba wanavalia njuga na kusimamia  ipasavyo suala la mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa na Halmashauri.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi Wilaya ya Bagamoyo yenye lengo la  kuona uhai wa chama pamoja na kuimarisha jumuiya zake zote sambamba na tenbelea miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba kumekuwepo na baadhi  changamoto ya utoaji wa fedha ambazo zinatolewa na mfuko wa Tasaf aziwafikii walengwa na zinakwenda kwa watu wengine ambao hawastahili

"Kuna malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi kuhusiana na suala la utoaji wa fedha ambazo zinatolewa na mfuko wa Tasaf zinakwenda kwa watu wengine ambao hawahusiki kabisa,"amebainisha Mwenyekiti huyo.

Kadhalika amesema kwamba fedha za asilimia kumi  ambazo zinatolewa kwa ajili ya makundi ya vijana,walemavu na wanawake zinatakiwa kutolewa kwa walengwa na sio kupewa watu wengine.

Akiwa katika chuo cha uuguzi na ukunga Mwenyekiti huyo amewahimiza wanafunzi hao kuzingatia maadili pamoja na kuwa wazalendo na nchi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga amempongeza  Mwenyekiti huyo  wa  Taifa kwa kufanya ziara hiyo ambayo itaweza kuleta matokeo chanya ya kimaendeleo. 

Pia Mkuu huyo wa Wiaya amebainisha kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 27 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bandari.
 
Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa amebainisha kwamba bado kuna changamoto ya migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo na kwamba wameshaanza kuifanyia kazi.

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Subira Mgalu  ameamua  kutoa  kiasi cha shilingi milioni 5  kupitia mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuweza kukarabati miundombinu ya majengo pamoja na uzio katika chuo cha uuguzi  na ukunga Bagamoyo.

Mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Pwani Jackson  KItuka amesema wataendelea kushirikiana na viongozi mbali mbali wa chama na serikali kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya CCM Taifa imeendelea katika Wilaya ya Bagamoyo ambapo imetembelea miradi mbali mbali ya maendelo ikiwemo chuo cha  uuguzi na ukunga,chuo cha kilimo kaole,kiwanda cha kuchakata taka hatarishi pamoja na  miradi  mbali ikiwemo Hospitali ya Chalinze na sekta ya elimu.

Post a Comment

0 Comments