Na Victor Masangu, Kibaha
Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Azania bank wameamua kuungana kwa pamoja na kuitoa darasa la mafunzo kwa wajasiriamali kutoka kata zote 14 kwa lengo la kuweza kuwapa ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbali mbali ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza katika ziara maalumu ya kikazi yenye lengo la kuweza kutoa mafunzo hayo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amebainisha kwamba ameamua kutoa darasa hilo ikiwa ni ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa zira ya kushukuru wanawake kwa kuweza kuipigia CCM kura za kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mwenyekiti Mgonja amesema kwamba ametembelea wanawake hao na kutoa fursa za mafunzo ya ujarisiamali kwa kuwafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa za aina tofauti zikiwemo utengenezaji wa sabubi kwa ajili ya kufulia nguo , sabuni ya kuogea, na namna ya kutengeneza batiki pamoja na utengenezaji wa bidhaa nyingine.
"Nikiwa kama Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini nimeamua kutimiza ahadi yangu ya kuwapa mafunzo ya ujariamali bure wanawake kutoka kata zote 14 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na mafunzo haya pia nimeshirikiana na wenzetu wa Azania bank ambao na wao wameweza kutoa elimu ya jinsi ya kutunza fedha na kujikwamua kiuchumi,"amebainisha Mwenyekiti Mgonja.
Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa Azania Bank Happiness Lema amebainisha kwamba lengo lao kubwa la kushirikiana bega kwa bega na Jumuiya ya ya wanawake wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini kwa lengo la kuwasaidia kuwapa elimu ya kujikwamua kichumi ikiwemo pamoja na suala zima la utunzaji wa fedha.
"Sisi kama Azania bank tumeoana kuna umuhimu mkubwa wa kuweza kushirikiana na Jumujiya ya wanawake wa UWT Wila ya Kibaha mjini na tumeamua kutembea nao katika ziara yakeo yenye lengo la kutoa darasa maaalumu kwa ajili ya kuwafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa na sisi kama benki tumewafundisha namna bora ya kujikomboa kiuchumi pamoja na jinsi ya kutumia fursa za mikopo yenye liba nafuu,"amenainisha Happiness.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini ya kutoa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali kwa sasa inaendelea kufanyika ambapo hadi sasa imeshapita katika kata tisa ambazo ni Msangani, Mkuza, Maili moja, Tumbi, Viziwaziwa, Kibaha, Kongowe, Misugususgu pamoja na Kata ya Visiga.
.jpeg)
.jpeg)
0 Comments