MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KIBAHA AAHIDI NEEMA YA KUWEKEZA KWA MKURUGENZI WA CLEOPATRA





Na Victor Masangu,Kibaha

Mstahiki Meya wa  Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dkt.Nicas Mawazo amewahakikishia wawekezaji ambao ni wazawa kuwapatia    maeneo kwa ajili ya uwekezaji mbali mbali kwa lengo la kuweza kutoa fursa za ajira kwa vijana na kukuza uchumi wa nchi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa halfa ya uzinduzi rasmi wa  sehemu maalumu iliyojengwa kwa ajili ya michezo mbali mbali ya kubahatisha iliyopo karibu na stendi ya zamani kata ya maili moja katika jengo la kontena bar Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

 Sehemu hiyo ambayo ni mradi mkubwa wa  Casino ya Kisasa ambayo inamilikiwa na kampuni inayotambulika kwa jina la  Cleopatra Tanzania yenye lengo la kuwapa fursa watu wa aina mbali mbali kucheza michezo ya kubahatisha.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mstahiki Meya  Dkt. Mawazo  amempongeza  mkurugenzi mkuu wa   CLEOPATRA Juma Mlali kwa kuweza kuwekeza katika mradi huo ambao utasaidia katika upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana na watu wengine.


Aidha amebainisha kwamba uwekezaji huo ni mkubwa na ni moja ya hatua za kuunga mkono  juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi kupitia uwekezaji ambao wameufanya.


Kadhalika Mstahiki Meya amesema kuwa akiwa meza kuu Mkurugenzi Mtendaji wa CLEOPATRA CASINO Juma Mlali amemweleza kuwa anatamani wapate eneo ili waweze kuwekeza kwa kujenga Kiwanda .

"Mimi nashukuru nimeshiriki katika halfa ya uzinduzi huu  na kiukweli  nimefurahishwa na juhudi zilizofanywa katika uwekezaji huu pia  nawakaribisha sana ofisini ili tuweze  kuwakopesha na kuwapa eneo la uwekezaji,"amebainisha Mstahiki Meya


Naye mkurugenzi mkuu  wa CLEOPATRA amebainisha kwamba wanajivunia kwa kutoa ajira kwa vijana wengi katika mikoa yote nchini .

"Tuna matawi nchi nzima na tumetoa ajira 400 na kwa upande wa uwekezaji tutaanza kujenga Kiwanda kwa ajili ya kutengeneza  vinywaji mbalimbali" amebainisha Mkurugenzi Mlali.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CLEOPATRA  Asha Simba  amesema kwa sasa wana maduka yapatayo  zaidi ya 53 ambayo yapo katika mikoa  mbali mbali ya Tanzania.

Nao baadhi ya vijana ambao walishiriki katiks uzunduzi huo wamepongeza juhudi za uwekezaji huo wa kuwepo na sehemu ya kisasa ambayo imetengwa kwa ajili ya michezo ya kubahatisha ambapo wameweza kupata fursa za ajira.

Post a Comment

0 Comments