Hiki ni choo cha kisasa ambacho hakimruhusu mtu kutoka chooni kama hajafanya usafi (flash) baada ya matumizi.
Hii ni Teknolojia inayouza Maji yenyewe bila muuzaji kuwepo.
NA MWANDISHI WETU
CHUO cha Uhandisi na Teknolojia cha Al-Maktoum kinashiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ambayo yamefunguliwa rasmi leo Machi 18, 2025 jijini Dar es salaam na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufikia kilele chake Machi 21 Mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa VETA katika Chuo hicho ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Umeme, Mhandisi Ramadhan Ruhulo amezungumzia kuhusu bunifu zao mbalimbali ambazo wamekuja kuzionesha katika maadhimisho hayo.
Miongoni mwa bunifu iliyokija kuoneshwa ni mfumo wa choo cha kisasa, ambacho kimeundwa mahsusi kwa ajili ya matumizi ya maeneo yenye mikusanyiko ya watu.
Mhandisi Ruhulo ameeleza kuwa Mfumo huo umebuniwa kwa kuzingatia usalama wa kiafya, ambapo mtumiaji hataruhusiwa kutoka nchini ya choo hicho bila kusafisha (flush) baada ya matumizi, kwani mlango wa choo hautafunguka hadi mtumiaji atakasafisha.
Bunifu nyingine ambayo ameielezea ni Teknolojia ya kuuzia Maji, ambapo Teknolojia hiyo inaweza kutoa huduma ya uuzaji wa Maji bila kuwepo Kwa mtu wa kusimamia kwani mteja atatumbukiza kiasi cha fedha kinachokidhi ujazo wa Maji anayotaka.
Kwamba ujazo Maji unaotakiwa ukifikiwa Teknolojia haitaendela kujaza bali itaacha kutoa Maji.
Aidha, Ruhulo amewahimiza wananchi kutothamini VETA kwa dhana potofu, bali kuitumia fursa ya mafunzo yanayotolewa ili kuongeza ujuzi wao, kama alivyoagiza Waziri Mkuu.
Pia amewakumbusha kuwa nafasi za kujiunga na chuo hicho bado zipo kwa kozi mbalimbali.
Kwa mawasiliano zaidi:
📞 0652-092-192
📞 0715-243-435 (Mratibu wa VETA Al-Maktoum College of Engineering and Technology & Mkuu wa Idara ya Umeme)


0 Comments