MASAUNI AJIVUNIA MAENDELEO JIMBO LA KIKWAJUNI KWA MIAKA MITANO



Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni. (Picha na Maktaba).

NA MWANDISHI WETU

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar na mtia nia wa ubunge jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi - CCM, Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amemshukuru Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa utekelezaji mkubwa wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020, suala lililowezesha Jimbo la Kikwajuni na Tanzania kwa ujumla kupiga hatua kubwa za Kimaendeleo.

Mhe. Masauni amebainisha hayo Agosti 19, 2025 wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye Jimbo la Kikwajuni pamoja na ahadi zake mbalimbali, akijivuni kasi kubwa ya maendeleo iliyopatikana katika huduma mbalimbali za Jamii, ikiwemo Ongezeko kubwa la huduma ya Maji safi na ya uhakika kwa wananchi pamoja na Ajira kwa Vijana.

"Nichukue fursa hii kuwashukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, vilevile na Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya na kuweza kufanikisha mambo mengi sana ya kimaendeleo katika Jimbo langu la Kikwajuni na Tanzania kwa ujumla. Jimbo langu la Kikwajuni sasa changamoto nyingi zimepungua." Amekaririwa Mhe. Masauni.

Mhandisi Masauni kadhalika amewashukuru wananchi wa Kikwajuni kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika kipindi chote akiwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, akisema ushirikiano huo wa wananchi umekuwa chachu ya kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni humo.

Post a Comment

0 Comments