WAZIRI mkuu mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne,Mizengo Pinda,atarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano kubwa la kimataifa la wafugaji wa Nguruwe Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Septemba 11 mpaka 13 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saalam.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Jiji Dar es salaam,Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa Nguruwe nchini,(TAPIFA)Dorine Maro,amesema kongamano hilo la kihistoria linalozungumzia mnyororo wa thamani kuhusiana masuala ya Nguruwe na sekta nzima.
"Ni kongamano ambalo halijawai kutokea nchini kwetu,ni mara ya kwanza,ni kongamano linalozileta nchi zote za Afrika hapa"Amesema Dorine.
Dorine amesema Kongamano ilo linatarajia pia kuwashirikisha wadau mbalimbali waliopo kwenye mnyororo wa thamani, wataalamu watakaowaeleza wafugaji Nguruwe kuhusu tafiti zilizofanywa.
Amesema vyama zaidi ya tisa Afrika wameshatbitisha kushiriki huku akihimiza wadau ambao wanataka kushiriki waweze kujisajili,pia akiwaomba makampuni ambayo yanataka kufadhili wajitokeze.
Akizungumzia hali ya ulaji wa nyama ya Nguruwe,Dorine amesema ulaji wake umeongezeka huku akiomba Serikali kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji hasa kwenye eneo la machinjio.
Kwa Upande wake Mdhamini wa kongamano ilo,Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),kupitia Meneja Masoko wa Benki hiyo,Richardi Stiveni,amewaimiza wafugaji wa Nguruwe kujitokeza kwenye kongamano ilo ili waweze kupata elimu ya Fedha na mikopo kubitia Benki hiyo.
0 Comments