Morogoro yafikiwa
Elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia imeendelea kuwafikia wananchi katika soko la Mahindi na vijiwe vya bodaboda waliopo Mikese Morogoro lengo likiwa ni kuhakikisha watu wanaachana na matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia kama vile kuni na mkaa.
Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) inaendelea na kampeni endelevu ya nishati safi ya kupikia ambapo tarehe 19 Februari 2026 kampeni hiyo iliwafikia wananchi katika Kata ya Mikese, wilaya ya Morogoro vijijini.
Timu ya uhamasishaji imekuwa ikizungumza na wananchi na wafanyabiashara ili kubaini nishati wanayotumia na kuwapatia elimu ya umuhimu wa kuhamia katika nishati safi.
Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa wanahitaji kutumia gesi zaidi wanapopika hivyo wameomba Serikali kuweka gharama rafiki za ununuzi wa nishati hiyo.
0 Comments