Na Victor Masangu, Pwani
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 imeamua kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na walipa kodi kwa kufanya usafi katika stendi ya mabasi chalinze pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya usafi kwa wafanyabiashara pamoja na kutoa vyombo mbali mbali vya kupikia kwa wakinamama ambao ni mama lishe.
Katika msafara huo ambao uliongozwa na Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Zanzibar Salehe Haji Pandu amesema kwamba wameamua kwenda kuwatembelea wafanyabiashara wa chalinze kwa lengo la kuweza kuwasaidia ili waweze kuhakikisha wanapiga hatua katika kutimiza ndoto zao.
"Katika kuelekea katika maadhimisho ya miaka 30 ya TRA tumeamua kwenda kufanya usafi katika stendi ya Chalinze ikiwa pamoja kugawa vifaa vya Usafi pamoja na Vyombo vya kupikia kwa Mama lishe pamoja na kuwawatembelea wafanyabiashara wa stendi ya Chalinze katika kutambua mchango wao kwa walipa kodi,"amebainisha Kamishna Haji.
Aidha Naibu Kamisha huyo amebainisha kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kiasi kikubwa inawategemea Wafanyabiashara hivyo ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara wanakua huku nguvu kubwa wakielekeza kwa wafanyabiashara walio nje ya wigo Kodi ili kuongeza idadi ya Walipakodi wengine Wapya.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Peter Eliona amessema kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega na na wafanyabiashara wote na kuwahimiza kuweka misingi ya kuweza kulipa kodi kwa wakati kwa lengo la kuiwezesha serikali kupata mapato yao.
Meneja Eliona amebainisha kwamba wameona kuna umuhimu mkubwa wa kwenda katika stendi hiyo ya mabasi chalinz e na kupata fursa ya kuzungumza na wafanyabiashara ikiwa pamoja na kufanya matendoya kugawa mahitaji mbali mbali ambayo yatawasaidia katika suala zima la utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo mama lishe pamoja na wafanyabiashara.
Naye Meneja wa Stendi ya Chalinze Henry Mwalugenge akizungumnza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze amewashukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutoa elimu ya Mlipakodi katika eneo hilo pamoja Vifaa vya Usafi ikiwani mojawapo ya kutengeneza mahusiano mazuri na Walipakodi.
Aidha Diwani wa Kata ya Bwilingu Laurence Peter amewapongeza TRA kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato na kurudisha kwa jamii itaongeza chachu ya Wafanyabishara kulipa kodi.
Akizungumnza kwa niaba ya Mama lishe Wa stendi ya mabasi chalinze,Mwenyekiti wa Mama lishe Bi.Zainabu Bakari amewashukuru TRA kwa kuwapa vifaa hivyo vitakavyo kwenda kuwarahisishia utendajikazi wao pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri kwa walipa kodi.
Mamlaka ya mappato TRA Mkoa wa Pwani imeamua katika kuelekea maadhimisho ya miaka 30 imeamua kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kufanya kongamano kwa walipa kodi na wadau, pamoja na kutembelea stendi ya mabasi chalinze na kugawa vifaa kwa wafanyabiashara, na mama lishe sambamba na kutoa elimu kwa mlipa kodi.



0 Comments