CONVOY OF HOPE YAANDAA MKAKATI WA KUIMARISHA ELIMU YA LISHE LONGIDO









NA MWANDISHI WETU, LONGIDO

Shirika la Convoy of Hope leo, Julai 23, 2026, limefanya kikao kazi cha maandalizi ya utekelezaji wa programu ya utoaji wa elimu ya lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, kikihusisha wataalamu kutoka halmashauri pamoja na wawakilishi wa shirika hilo.

Kupitia mradi wake wa lishe, Convoy of Hope imekuwa ikifanya tathmini ya hali ya lishe kwa watoto katika maeneo ya utekelezaji wa mradi, kwa lengo la kubaini watoto wenye changamoto za lishe, hususan utapiamlo, ili waweze kupata huduma stahiki kwa wakati.

Katika kikao hicho, wadau walijadili na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa elimu ya lishe katika vituo vya mradi, pamoja na kuboresha utaratibu wa kuwaunganisha watoto watakaobainika kuwa na changamoto za lishe na watoa huduma za afya.

Hatua hiyo inalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu lishe bora, kuboresha afya za watoto na kupunguza athari za utapiamlo katika Wilaya ya Longido.


Post a Comment

0 Comments